Wafungwa 41 Wateketezwa na Moto Gerezani Wakiwa Wamelala
Wafungwa wapatao 41 wamefariki dunia baada ya moto kutekeza gereza moja nchini Indonesia, pembezoni mwa mji mkuu wa Jakarta. Inaripotiwa kuwa moto huo ulitokea mapema asubuhi siku ya Jumatano, Septemba 8, katika Gereza la Tangerang wakati wafungwa hao walikuwa wamelala.